Proverbs 25:2-7

2 aNi Utukufu wa Mungu kuficha jambo,
bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo.

3Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini,
ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki.

4 bOndoa takataka kwenye madini ya fedha,
nako ndani yake kutatokea chombo
cha mfua fedha.
5 cOndoa waovu mbele ya mfalme,
nacho kiti chake cha enzi
kitaimarishwa kwa njia ya haki.

6Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme,
wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu;
7 dni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,”
kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu.

Kile ulichokiona kwa macho yako
Copyright information for SwhNEN